DJI AGRAS T40

DJI AGRAS T40 ni droni ya kilimo yenye uwezo mkubwa, iliyoundwa kuboresha shughuli za kilimo kwa ufanisi na usahihi. Ikiwa na muundo wa kipekee wa rotori mbili, AGRAS T40 inaweza kubeba mzigo wa kunyunyizia wa kilo 40 na mzigo wa kusambaza wa kilo 50 (lita 70), ikiongeza uwezo wa kubeba mzigo kwa asilimia 30.

Mfumo wa Kunyunyizia

AGRAS T40 ina Mfumo wa Kunyunyizia wa chembechembe Mbili unaotoa kiwango cha mtiririko wa lita 12 kwa dakika. Muundo mpya wa pampu ya sumaku hutenganisha kabisa dawa na motor, kuifanya ndege kutopata kutu na kudumu kwa muda mrefu.

Mfumo wa Kusambaza

Ikiwa na uwezo wa kubeba mzigo wa kusambaza wa kilo 50, AGRAS T40 ina mfumo ulioimarishwa wa kusambaza unaojumuisha sensa ya mzani inayofuatilia kiasi kinachosambazwa, na mzigo uliobaki kwa wakati halisi.

Mfumo wa Radar na wa Kuona

AGRAS T40 imeunganishwa na Active Phased Array Radar pamoja na mfumo wa kuona wa binocular, unaotoa utambuzi wa vikwazo kwa pande zote kwa nyuzi 360. Mfumo huu unaruhusu ndege kufuatalia ardhi kwa akili, kupita na kuepuka vikwazo kwa umbali wa hadi mita 50, hivyo kuhakikisha usalama wa hali ya juu katika operesheni.

Uchoraji Ramani na Udhibiti

Droni hii inawezesha uchoraji wa ramani, kunyunyizia, na kusambaza, yote katika kifaa kimoja. Kamera ya UHD na gimbal, huruhusu upigaji wa picha za shamba na bustani kwa wakati halisi, na ramani za eneo zinaweza kuzalishwa kwa kutumia muunganisho wa mtandao maalum. Mfumo hutambua mipaka ya ardhi na vikwazo kiotomatiki, hivyo kurahisisha upangaji wa njia za ndege juu ya mashamba na bustani zenye milima.

Rimoti ya mbali

Kidhibiti cha mbali kimeboreshwa kikamilifu kwa ajili ya uchoraji wa ramani ulio laini na wa haraka zaidi. Kinawezesha uchoraji wa ramani wa hekta 6.67 kwa dakika 10, kikipunguza safari zisizo za lazima kwa upangaji wa njia za ndege hii, hivyo kuongeza ufanisi. Kioo kikubwa cha inchi 7 chenye mwangaza wa hali ya juu inatoa mwonekano mpana na maelezo yaliyo wazi.

Uimara na Utendaji

Vipengele vya msingi vya AGRAS T40 vimeundwa kuhimili mazingira magumu na changamoto za kilimo. Vimepitia majaribio makali kama vile kuzuia kutu, joto la juu na la chini, na majaribio ya kuchakaa, kuhakikisha uimara na kutegemewa kwa muda mrefu.

Kwa ujumla, DJI AGRAS T40 ni suluhisho la kina kwa wakulima wanaotafuta kuongeza ufanisi, usahihi, na usalama katika shughuli zao za kilimo.