DJI Agras T20P – Droni ya Kilimo Inayoboresha Ufanisi na Usahihi

DJI Agras T20P ni droni ya kisasa ya kilimo iliyoundwa ili kuboresha ufanisi na usahihi katika shughuli za kilimo cha kisasa. Kwa muundo wake mwepesi na unaobebeka kwa urahisi, T20P inaweza kubeba mzigo wa kunyunyizia wa hadi kilo 20 na mzigo wa kusambaza wa hadi lita 35 (kilo 25), na kuifanya kuwa kifaa kinachofaa kwa matumizi mbalimbali shambani chenye kumaliza hecta 12 kwa saa moja kwa shamba, hecta 2.6 kwa bustani ya matunda, na kusambaza ton 1 ya mbolea kwa saa moja, kulingana na mahitaji tofauti ya mazingira husika.

Mfumo wa Kunyunyizia Chembechembe mara Mbili

Ikiwa na mfumo wa kunyunyizia chembechembe mara mbili, Agras T20P kuhakikisha matone ya dawa yanagawanyika kwa usawa, jambo linaloongoza ufanisi wa kunyunyizia viuatilifu huku ikipunguza upotevu wa dawa na athari kwa mazingira.

Mfumo wa Kisasa wa Kuepuka Vikwazo

Droni hii imejumuishwa na teknolojia ya Active Phased Array Radar pamoja na mfumo wa kuona yaani binocular, ambayo hutoa uwezo wa hali ya juu wa kugundua na kuepuka vikwazo. Teknolojia hii huwezesha Agras T20P kuruka kwa usalama hata kwenye maeneo yenye vikwazo vingi au ardhi isiyo tambarare.

Uwezo wa Kuchora Ramani na Kufanya Uchunguzi

Mbali na kunyunyizia na kusambaza, Agras T20P pia inaweza kutumika kwa ajili ya uchunguzi, ukusanyaji wa taarifa na uchoraji wa ramani. Kamera yake ya FPV ya ubora wa juu, yenye gimbal inaweza kugeuka, hutoa picha za wakati halisi kwa urahisi, kurahisisha uchoraji wa ramani za mashamba na bustani kwa ustadi mkubwa.

Uendeshaji Rahisi kwa Mtumiaji

Imeundwa kwa kuzingatia urahisi wa matumizi, Agras T20P hutoa vidhibiti vinavyofaa mtumiaji na vipengele vinavyorahisisha matengenezo. Muundo wake wa kimoduli huruhusu kuikunja kwa haraka, hivyo kupunguza muda wa mapumziko na kuongeza tija wakati wa shughuli za shambani.

Kwa ujumla, DJI Agras T20P ni droni ya kilimo yenye uwezo mkubwa na utendaji wa hali ya juu. Inatoa suluhisho bora kwa wakulima wanaotaka kuongeza ufanisi katika kunyunyizia, kusambaza, na kuchora ramani kwa usahihi na kwa haraka.