DJI Agras T50

DJI Agras T50 ni droni ya kilimo ya kisasa iliyoundwa kuboresha mbinu za kilimo cha kisasa. Kwa uwezo wake mkubwa na teknolojia ya hali ya juu, Agras T50 inatoa ufanisi wa pekee na usahihi katika usimamizi wa mazao.

Sifa Muhimu:

Uwezo Mkubwa wa Kubeba Mizigo: Inaweza kubeba hadi kilo 40 kwa kunyunyizia, na hadi kilo 50 kwa kusambaza mbegu au mbolea, hivyo kufanikisha kumaliza eneo kubwa kwa muda mfupi.

Mfumo wa Kunyunyizia wa chembe chembe: Hutoa kiwango cha juu cha mtiririko wa hadi lita 16 kwa dakika kwa kutumia vinyunyizo viwili, na hadi lita 24 kwa dakika kwa vinyunyizo vinne, kwa ufanisi mkubwa.

Uchunguzi wa mazingira yenye vizuizi kwa mfumo wa Kisasa: Ina rada za pande zote za mbele na nyuma pamoja na mfumo wa kuona wa macho mawili (binocular vision), unaoiwezesha kugundua vizuizi kwa pande nyingi na kufuata kimo cha ardhi kwa usalama zaidi wakati wa operesheni.

Ufanisi Mkubwa wa Utendaji: Ina uwezo wa kumaliza hadi hekta 21 kwa saa wakati wa operesheni za shambani na kusambaza hadi kilo 1,500 za punje kwa saa, hivyo kuongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.

Uwezo wa kutambua vikwazo na kutumika kwenye miinuko: inaweza kutumika kwenye mashamba ya miinuko na ya matunda na vile vile ina uwezo wa kukwepa vikwazo kwa ustadi na ufanisi wa hali ya juu. Hivyo kuongeza usahihi na ustadi mkubwa katika kunyunyizia katika miinuko na mazao ya miti ya matunda.

Picha ya miinuko na mabonde ya ardhi ikipimwa kwa rada.

DJI Agras T50 imetengenezwa kukidhi mahitaji mbalimbali ya kilimo cha kisasa, ikiwaruhusu wakulima kutumia suluhisho la kuaminika na la ufanisi kwa kazi za kunyunyizia na kusambaza. Droni hii ina muundo imara yenye nyenzo na uimara ili  kuongeza uzalishaji na kuhakikisha afya bora ya mazao.